Saturday, July 9, 2016

Kujiunga na bima ya afya kwa watoto chini ya miaka 18

1. Tembelea ofisi za bima ya afya zilipo karibu na wewe na kuchukua fomu kwa ajili ya usajili
2. Unajaza fomu utakazopatiwa ikiwapo na picha mbili za mtoto husika
3. Unachukua account namba na kwenda bank kulipia kiasi cha Tsh 50,0400 kwa ajili ya kujiunga na bima ya mtoto chini ya miaka 18
4. Baada ya kulipia bank unarudisha fomu katika ofisi ya bima ukiambatanisha na fomu ya maombi
5. Baada ya hapo utasubiri kwa muda usiopungua wiki 4-6 kuweza kupatiwa kadi yako
6. Unakuwa unasibiri kupata kadi ya matibabu endapo utahitaji kwenda hospital una haki ya kupata matibabu chini ya mfuko wa bima ya afya hivyo basi unatakiwa kutembelea ofisi ya bima iliyopo karibu na wewe kwa ajili ya kupata fomu ya matibabu mpaka utakapopata kadi yako ya matibabu.